Vyama vya Sudan Kusini vyafanya mazungumzo ili kuondoa mvutano kuhusu usalama
2022-04-01 08:45:31| CRI

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na makamu wake wa kwanza Bw. Riek Machar wanafanya majadiliano ili kumaliza mvutano juu ya mipango ya usalama.

Bw. Bol Makueng, katibu wa masuala ya ndani wa Chama cha SPLM kinachoongozwa na rais Kiir, amesema viongozi hao wanashauriana kuhusu namna ya kusonga mbele kwenye utekelezaji wa amani.

Machi 22, Chama kikuu cha upinzani SPLM/A-IO kinachoongozwa na Bw. Machar kilijitoa kwenye mipango ya usalama, kikilaani mashambulizi “yasiyo na sababu” dhidi ya vituo vyake yaliyofanywa na vikosi vya ulinzi vya Sudan Kusini (SSPDF).

Chama hicho pia kilikataa nafasi tatu ndani ya jeshi na polisi zilizotolewa kwake na rais Kiir.