Riwaya ya Mbali na Nyumbani
2022-04-01 14:17:40| cri

Riwaya ya Mbali na Nyumbani_fororder_微信图片_20220401141726


Mbali na Nyumbani ni riwaya ya kitawasifu inayosimulia ari ya mhusika mkuu ya kukisaka ikipendacho roho. Ukosapo mapenzi utaondoka nyumbani uende mbali ukayasake; ukosapo masomo utafanya vivyo hivyo. Ukosapo marafiki au kazi utajipata barabarani ukitamba na njia kwenda kuisaka. Je, unaposukumwa na ari au utundu wa kitoto utaenda mbali na nyumbani kuukomesha utundu huo na kuizima kiu ya kujua usiyoyajua? Kama ni kutafuta maarifa, hiyo ni heri... mpaka safari igeukapo kuwa na shari ndipo utakapobaini ukweli kwamba nyumbani hamna mfanowe hata pawe ni pangoni.