Kiongozi wa Kenya aahidi kuwekeza katika mafunzo ya kijeshi ili kuzuia matishio ya usalama
2022-04-01 09:29:52| CRI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuendelea kuwekeza katika kufanya mafunzo yawe ya kisasa ili kusaidia vikosi vya usalama vya nchi hiyo kuwa na utaalamu wa kutosha kukabiliana na changamoto zinazoletwa na matishio yanayobadilika.

Rais Kenyatta amesema ushirikiano katika elimu na mafunzo utaimarisha mshikamano wa idara za usalama za nchi hiyo, na kuhimiza mbinu shirikishi za operesheni ambazo zimethibitishwa kuwa na mafanikio katika kutatua masuala ya usalama.

Nchi hiyo inachunguza bajeti zisizowekwa wazi kwa ajili ya mafunzo ya vikosi vyake vya usalama na kutoa vifaa vya kisasa kusaidia kukabiliana na matishio ya usalama yanayoibuka nchini humo. Uwekezaji huo utaviwezesha vikosi vya usalama kupata mafunzo maalumu ya mwaka mzima, ili kupambana na uhalifu wa kupangwa wa kuvuka mipaka unaoendelea.