Waziri wa mambo ya nje wa China aendesha mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa majirani wa Afghanistan
2022-04-01 08:59:06| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameendesha mkutano wa tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani za Afghanistan, uliofanyika mkoani Anhui.

Kwenye mkutano Bw. Wang alisoma ujumbe kutoka kwa Rais Xi Jinping na kuongea kwa niaba ya upande wa China. Amesema kwa sasa Afghanistan iko kwenye njia panda ya historia, na nchi jirani zimeanzisha uratibu na njia za ushirikiano, na kuweka maafikiano ya kisiasa ili kushirikiana kujibu mabadiliko kwenye hali ya Afghanistan.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoshiriki kwenye mkutano huo wamemshukuru Rais Xi kwa ujumbe aliotoa kwa mkutano huo, ambao umetajwa kuwa umeongeza msukumo wa ushirikiano kati ya nchi jirani za Afghanistan. Pia wamepongeza mchango wa China kuzileta pamoja nchi hizo na kuunga mkono ujenzi mpya wa amani wa Afghanistan.