Tanzania na wenzi wake wa maendeleo kuzindua mradi wa ulinzi wa ustawi wa vijana
2022-04-04 08:32:29| CRI

Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) na Uswisi zitazindua mradi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 5.1 unaolenga kulinda vijana kwa kuboresha afya na ustawi wao.

Mchambuzi wa miradi wa UNFPA, Fatina Kiluvia amesema jana jijini Dar es Salaam kuwa, vijana, wanaochukua nafasi muhimu katika maendeleo yoyote endelevu, wanahitaji kutunzwa na kuwezeshwa ili kutimiza uwezo wao katika kukabiliana na vizuizi vingi ambavyo viawazuia kutimiza malengo yao.

Amesema UNFPA kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na serikali ya Uswisi zimeandaa mpango wa miaka mitatu unaolenga kutengeneza mazingira mazuri ya kiuchumi na kijamii, kisheria, na sera na kujenga uwezo kwa watoto chini ya miaka 18 na vijana.

Kwa upande wake, mwakilishi wa UNFPA nchini Tanzania Mark Schreiner amesema, mradi huo utakaotekelezwa Tanzania bara na Visiwani utaanza leo jumatatu.