Watu 12 wauawa katika ghasia kwenye gereza nchini Ecuador
2022-04-04 08:20:07| CRI

Waziri wa mambo ya ndani wa Ecuador Patricio Carrillo amesema, watu 12 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika ghasia zilizotokea mapema jana kwenye gereza la mji wa Cuenca.    waziri huyu amesema, ghasia hiyo ilisababishwa na mapambano kati ya makundi ya wafungwa, na hivi sasa polisi na vikosi vya usalama vimeingia kwenye gereza hilo na kudumisha utaratibu.