Watu 6 wauawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa California
2022-04-04 08:37:20| cri

Takriban watu 6 wameuawa na wengine 9 kujeruhiwa katika tukio la ufyatuaji risasi huko Sacramento, mji mkuu wa California, nchini Marekani tarehe 3 alfajiri kwa saa za huko.

Polisi wa eneo hilo wamesema,mtu mmoja asiyejulikana alifyatua risasi kwa watu nje ya mgahawa mmoja katikati ya mji huo, na mshukiwa huyo alitoroka baada ya kufanya shambulizi hilo.