Mjumbe wa China atoa wito wa kuzingatia maendeleo
2022-04-04 09:53:03| CRI

Mjumbe wa China atoa wito wa kuzingatia maendeleo_fororder_戴兵

Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Dai Bing ametoa wito kwa Kundi la Nchi 20 (G20) kufanya maendeleo kuwa kipaumbele cha kwanza katika ushirikiano.

Balozi Dai amesema, hiki ni kipindi muhimu cha kupambana na janga la COVID-19 na kufufua uchumi, huku dunia ikikabiliwa na misukosuko katika nyanja mbalimbali. Ameongeza kuwa kama jukwaa kuu la ushirikiano wa kimataifa wa kiuchumi na jukwaa muhimu la usimamizi wa mambo ya kiuchumi duniani, G20 inabeba majukumu muhimu. Pia linapaswa kuimarisha mshikamano, ushirikiano, mawasiliano na uratibu, kufuatilia masuala muhimu ya kiuchumi na kifedha, kuweka kipaumbele cha ushirikiano katika maendeleo, na kukabiliana kwa pamoja changamoto kubwa za afya, dijitali na nishati duniani.

Balozi Dai amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kuunga mkono kazi ya Indonesia ambayo ni mwenyekiti wa zamu wa G20, kuhimiza mafanikio ya Mkutano wa Bali, na kutoa mchango kwa kuboresha usimamizi wa uchumi duniani na kuhimiza kufufuka kwa uchumi wa dunia.