Tanzania yazindua mradi mkubwa wa mageuzi ya kilimo
2022-04-05 08:37:24| CRI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua mradi mkubwa wa mageuzi ya kilimo unaolenga kukabiliana na changamoto katika sekta hiyo na kuiwezesha nchi hiyo kujitosheleza kwa chakula.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, rais Samia amesema utawala wake umeongeza bajeti kwa ajili ya utafiti, uzalishaji wa mbegu na huduma husika ili kuboresha uzalishaji wa kilimo, na kuongeza kuwa Tanzania pia inatafuta masoko ya mazao yake ya kilimo katika nchi za nje. Amesema mipango inaendelea ya kujenga maghala ya kuhifadhi mazao katika maeneo ya vijijini ili kudhibiti upotevu unaotokea baada ya mavuno.

Rais Samia ameitaka sekta binafsi za ndani na nje ya nchi pamoja na wenzi wa maendeleo kuunga mkono mradi huo ili kuwezesha kutimiza malengo yake.