UM waahidi kuondoa matishio ya mlipuko nchini Somalia
2022-04-05 08:23:18| CRI

Umoja wa Mataifa jana umeahidi kuunga mkono Somalia kuondoa matishio ya mlipuko na kusisitiza athari ya mlipuko kwa watu. Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Somalia James Swan, amesema Umoja huo una nia ya kuongeza uwezo wa nchi mbalimbali kukabiliana na matishio ya vifaa vya mlipuko kwa njia endelevu. 

Bw. Swan aliyasema hayo katika shughuli za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mabomu ya kutegwa ardhini, ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni “ardhi salama, hatua salama na nyumba salama”. 

Amesema kuwa, uchafuzi unaosababishwa na mabaki ya vifaa vya mlipuko na mabomu ya kutegwa ardhini, na mgogoro wa miaka mingi vitaendelea kuleta athari kwa usalama wa binadamu, na kuzuia juhudi za maendeleo.