Wadhamini wa amani nchini Sudan Kusini wataka pande husika kuweka nia halisi ya kutatua masuala ambayo hayajapata ufumbuzi
2022-04-06 08:48:05| CRI

Nchi Tatu za Magharibi zinazodhamini amani nchini Sudan Kusini zimepongeza uamuzi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, SPLM/A-IO wa kushiriki tena kwenye mpango wa amani, na kutoa wito wa nia halisi ya kutatua masuala ambayo bado hayajapata ufumbuzi.

Katika taarifa yao ya pamoja iliyotolewa katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, Marekani, Uingereza, na Norway, ambazo ni wajumbe wa udhamini wa amani, wamepongeza pande husika kufuatia makubaliano waliyofikia hivi karibuni ya kuendelea na utekelezaji wa mipango ya usalama iliyowekwa ili kurejesha uhai kwenye makubaliano ya amani.

Wachambuzi wanasema, kutofikia makubaliano kuhusu muundo wa vikosi vya pamoja ni moja ya masuala muhimu ya kiusalama ambayo yanachelewesha utekelezaji wa makubaliano ya amani ya mwaka 2018.