China yatarajia vita ya Ukraine itasimamishwa mapema
2022-04-06 09:17:55| CRI

China yatarajia vita ya Ukraine itasimamishwa mapema_fororder_张军

Mwakilishi  wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema, kuhimiza kupunguza hali ya wasiwasi, na kusimamisha vita nchini Ukraine ni tarajio la haraka la jumuiya ya kimataifa, na pia ni tumaini kubwa la China.

Balozi Zhang amesema hayo kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Ukraine. Amesema China imesisitiza mara kwa mara kuwa mazungumzo ni njia pekee ya kufungua mlango wa amani, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuweka mazingira mazuri kwa mazungumzo kati ya Russia na Ukraine, badala ya kuweka vikwazo na kuchochea migogoro, ili kuzuia hali ya wasiwasi isizidi kuwa mbaya.

Balozi Zhang amesema, China inatilia maanani sana suala la haki za binadamu nchini Ukraine, na kuunga mkono mapendekezo na hatua zote zinazoweza kupunguza hali ya wasiwasi ya kibinadamu, na  aliongeza kuwa, China itaendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Ukraine na nchi zake jirani.