Mafanikio ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya CMG yatia nuru Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing
2022-04-07 19:47:24| Cri

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC hivi karibuni imetumia barua Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, ikitoa pongezi na shukrani kwa CMG kuitangaza kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na harakati za Olimpiki za Kimataifa.

Ingawa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na ya Walemavu ya mwaka 2022 imefungwa, lakini utangazaji wenye ubora wa juu wa michezo hiyo bado yanasifiwa duniani. Mafanikio ya uvumbuzi wa sayansi na teknolojia ya CMG yaliyotumiwa kwenye utangazaji huo yametia nuru michezo hiyo, kuwekwa katika kumbukumbu ya Olimpiki.