Thamani ya jumla ya uzalishaji wa baharini yazidi yuan trilioni 9
2022-04-07 08:15:06| CRI

Taarifa ya takwimu za uchumi wa baharini wa China kwa mwaka 2021 iliyotolewa na Wizara ya Maliasili ya China inaonyesha kuwa, mwaka 2021, thamani ya jumla ya uzalishaji wa mazao ya baharini nchini China imezidi yuan trilioni 9 (sawa na dola za kimarekani bilioni 1.4), na kuchangia asilimia 8 katika ongezeko la uchumi la China.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa, uwezo wa utafiti na utengenezaji wa vifaa vya ngazi ya juu vya baharini umeongezeka zaidi, na baadhi ya teknolojia zenye uvumbuzi za uchumi wa baharini zimefikia kiwango cha juu cha kimataifa.