Katibu mkuu wa UM apongeza kuanzishwa kwa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia
2022-04-07 08:35:55| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana amepongeza kuanzishwa karibuni kwa Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS).

Katika taarifa yake, Bw. Guterres amesisitiza uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia, pia amesema anaunga mkono kikamilifu Tume hiyo na vikosi vya usalama vya Somalia kupambana na kundi la al-Shabab.

Bw. Guterres pia amewataka washirika wote wahakikishe ufadhili endelevu wa kifedha kwa Tume hiyo na kutoa vifaa vinavyohitajika kwa vikosi vya usalama wa Somalia, ili kuunga mkono mpito wa usalama wa nchi hiyo.