Wakimbizi wenye asili ya Afrika kutoka Ukraine washuhudia ubaguzi wa rangi nchini Marekani
2022-04-07 08:36:55| CRI

Marekani imeendelea kuwarudisha makwao wakimbizi wenye asili ya Afrika na Caribbean wanaoingia nchini humo wakikimbia mapigano nchini Ukraine, na kuwafanya wakimbizi hao kulichukua suala hilo kama ubaguzi wa rangi.

Mwezi uliopita, rais wa Marekani Joe Biden alitangaza mpango wa kuwapokea raia 100,000 wa Ukraine wanaokimbia mapigano nchini mwao, na kutoa hadhi ya ulinzi wa muda kwa Waukraine wengine 30,000 ambao tayari walikuwa nchini Marekani, na kusitisha kuwarejesha raia wa Ukraine nchini kwao.

Hata hivyo, wakimbizi wenye asili ya Afrika walionyesha wasiwasi wao kutokana na wakimbizi raia wa Haiti kurejeshwa nchini mwao, na mapokezi mabaya ya wakimbizi wenye asili ya Afrika na Mashariki ya Kati ikilinganishwa na mapokezi wanayopewa raia wa Ukraine.