WHO yasema dawa za mitishamba za kichina zinaweza kutibu COVID-19
2022-04-07 08:53:23| CRI

WHO yasema dawa za mitishamba za kichina zinaweza kutibu COVID-19_fororder_VCG111284116924

Shirika la Afya Duniani (WHO) hivi karibuni limetoa ripoti kuhusu ufanisi wa matibabu na dawa za mitishamba za kichina katika kutibu COVID-19, na kuhimiza nchi wanachama wa Shirika hilo kufikiria uwezekano wa kutumia matibabu na dawa hizo.

Kwa muhibu wa ripoti hiyo, matabibu na dawa za kichina zinaweza kutibu watu walioambukizwa COVID-19, haswa wale wenye dalili ndogo na za kawaida, na kupunguza hatari ya kugeuka kuwa na dalili kali.

Ripoti hiyo imepongeza serikali na watafiti wa China kwa kutoa mchango katika kuongeza elimu na kuendeleza mbinu ya kutibu COVID-19, na kusema kuna haja ya kuendelea na utafiti wa matibabu na dawa za mitishamba za kichina katika kutibu COVID-19.