Rais Xi atoa hotuba muhimu katika Mkutano wa kutoa pongezi kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing
2022-04-08 14:43:42| Cri

Mkutano wa majumuisho na kutoa pongezi za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing umefanyika leo asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa Beijing ambapo rais Xi Jinping ametoa hotuba muhimu.

Katika hotuba yake rais Xi amesema baada ya miaka saba ya kazi ngumu, Michezo hii ilifanyika kwa mafanikio na kuvutia ufuatiliaji wa nchi nzima na dunia. Watu wa China pamoja na watu wa nchi nyingine, wameshinda shida na changamoto tofauti, na kwa mara nyingine tena wamefanya Michezo ya Olimpiki ambayo itakumbukwa katika historia, na kuwa na utukufu wa Olimpiki kwa pamoja. Amesema ukweli umedhihirisha tena kuwa Wachina wana dhamira ya kuchangia maendeleo ya harakati za Olimpiki na umoja na urafiki wa watu duniani, na wana uwezo na matumaini ya kuendelea kutoa mchango mpya na mkubwa.

Katika mkutano huo, Kamati Kuu ya Chama na Baraza la Serikali la China zimeamua kutunuku vitengo na watu 148, nishani ambazo zimetolewa na rais Xi Jinping na viongozi wengine wa serikali.