China yapongeza pande husika za Sudan Kusini kukubaliana kuhusu mpango wa usalama wa kipindi cha mpito
2022-04-08 08:52:40| cri

China yapongeza pande husika za Sudan Kusini kukubaliana kuhusu mpango wa usalama wa kipindi cha mpito_fororder_赵立坚

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Zhao Lijian jana alisema, China inazipongeza pande husika nchini Sudan Kusini kwa kufikia makubaliano ya mpango wa usalama katika kipindi cha mpito, ambayo ni hatua nyingine muhimu katika mchakato wa amani nchini humo.

Bw. Zhao amesema, China inatumai kuwa pande hizo zitatekeleza kwa hatua halisi maudhui husika ya makubaliano hayo na kusukuma mbele mchakato wa mpito wa kisiasa nchini Sudan Kusini, ili kufikia amani na utulivu wa muda mrefu nchini humo.