Xi ahudhuria mkutano wa kupongeza Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi Beijing na ya Walemavu
2022-04-08 11:13:42| Cri

Rais Xi Jinping wa China leo asubuhi amehudhuria mkutano uliofanyika hapa Beijing ili kuwasifu watu waliotoa mchango mkubwa katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing 2022.

Serikali ya China imetoa sifa ya heshima kwa makundi 148 na watu 148, ikiwa ni pamoja na mtu mmoja aliyefariki dunia, kuwa ni “Makundi yaliyotoa mchango mkubwa”na“Wtu waliotoa mchango mkubwa” kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing 2022.