Peter Kagwanja: mazungumzo kati ya China na Afrika yanachochea maendeleo ya pamoja
2022-04-11 09:55:35| cri

Peter Kagwanja: mazungumzo kati ya China na Afrika yanachochea maendeleo ya pamoja_fororder_QQ图片20220411110111

Mazungumzo na maelewano kati ya China na Afrika yanachochea maendeleo kwa kanda zote mbili.

Hayo yamesemwa na Peter Kagwanja, mtendaji mkuu wa Taasisi ya Sera ya Afrika yenye makao makuu mjini Nairobi katika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Nation siku ya Jumapili.

Mtaalamu huyo alisema katika karne ya 21, China na Afrika zimeazimia kufika mbali na kwa pamoja. Alisema, pande hizi mbili zilikumbatia ushirikiano, uhusiano wa kiwenzi wenye usawa na mshikamano ili kuimarisha uhusiano wao katika utaratibu wa kimataifa wenye msukosuko.

Kwa mujibu wa Kagwanja, uhusiano kati ya China na Afrika kwa sasa umejengwa juu ya historia ndefu ya maelewano kati ya pande hizo mbili. Alibainisha kuwa tangu enzi za mafarao katika Misri ya kale, mabaharia na wafanyabiashara wa China walisafiri kwenda Afrika na vile vile wasomi na wasafiri wa Afrika pia walitembelea China.

Alieleza kuwa baada ya historia ndefu ya uvamizi, unyonyaji na udhalilishaji kutoka nje, pande hizi mbili zimeweka upya mpango na kuunda tena Njia ya kale ya Hariri kama barabara kuu mpya ya mazungumzo baina ya pande mbalimbali katika zama za utandawazi.