Rais Xi asisitiza umuhimu wa “mbegu za China” katika kuhakikisha usalama wa chakula
2022-04-11 16:10:58| cri

Rais Xi Jinping wa China jana jumapili alisisitiza umuhimu wa “mbegu za China” katika kuhakikisha usalama wa chakula.

Akifanya ziara ya ukaguzi katika maabara ya mbegu mjini Sanya mkoani Hainan, Rais Xi amebainisha kuwa usalama wa chakula wa China unaweza kuhakikishwa wakati raslimali za mbegu zinadhibitiwa kithabiti na wachina.

Rais Xi amesisitiza kuwa ili kuhakikisha kuwa raslimali za mbegu za China zinakuwa chini ya udhibiti bora, lengo la kujitegmea lazima litimizwe kwenye teknolojia ya mbegu.

Rais Xi ametoa wito wa kufanywa juhudi endelevu ili kuendeleza sekta ya mbegu ya China.