China yatoa mwongozo wa kuanzishwa soko la pamoja la ndani
2022-04-11 09:53:17| cri

China yatoa mwongozo wa kuanzishwa soko la pamoja la ndani_fororder_VCG111377176428

China imetoa mwongozo wa kuharakisha kuanzishwa soko la pamoja la ndani ambalo litakuwa na ufanisi wa juu zaidi, linalofuata sheria, zuri kwa ushindani, na lenye uwazi.

Mwongozo huo uliotolewa kwa pamoja na Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali unafafanua zaidi kuwa, China inalenga kuhimiza mzunguko na upanuzi unaofaa wa soko la ndani, kukuza utulivu, haki, uwazi na mazingira ya biashara yanayotabirika, na kupunguza gharama za miamala ya soko. Zaidi unalenga kusukuma mbele uvumbuzi wa sayansi na teknolojia na kuboresha sekta pamoja na kuibua faida mpya za kuingia kwenye ushindani na ushirikiano wa kimataifa.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, juhudi zitachukuliwa ili kuboresha mfumo wa pamoja wa ulinzi wa hakimiliki, kutekeleza mfumo wa upatikanaji wa soko la pamoja, na kuboresha mfumo wa pamoja wa mikopo ya kijamii.