Mawaziri wa Umoja wa Ulaya washindwa kutoa uamuzi kuhusu vikwazo dhidi ya mafuta ya Russia
2022-04-12 09:03:33| cri

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya washindwa kutoa uamuzi kuhusu vikwazo dhidi ya mafuta ya Russia_fororder_欧盟俄罗斯石油禁运

Mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya nje na sera ya usalama Josep Borrell amesema, mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya bado hawajatoa uamuzi juu ya vikwazo vinavyolenga mafuta na gesi ya Russia.

Akihutubia vyombo vya habari baada ya Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Luxemburg, Borrell amesema ingawa uamuzi bado haujatolewa, “hakuna kilichoondolewa, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya mafuta na gesi.” Mwaka jana, bili ya mafuta ilikuwa mara nne kuliko gesi, “kwa hiyo ni muhimu kuanza na mafuta.”

Alieleza kuwa vikwazo hivi vitasababisha “athari zisizo na usawa” kati ya nchi za Umoja wa Ulaya kwa kuwa nchi wanachama wa Ulaya ya Kati na ya Mashariki “zinategemea sana” uagizaji wa nishati kutoka Russia.

Pia alitupilia mbali madai ya Russia kwamba kuongezeka kwa upungufu wa chakula kunatokana na vikwazo dhidi ya Russia. Badala yake, aliishutumu Russia kwa “kuchochea njaa duniani.”