Watu 20 wajeruhiwa New York katika shambulizi la ufyatuaji risasi kwenye subway
2022-04-13 09:06:27| cri

Watu 20 wajeruhiwa New York katika shambulizi la ufyatuaji risasi kwenye subway_fororder_纽约枪击

Watu 20 walijeruhiwa, wakiwemo 10 wenye majeraha ya risasi, katika shambulio la treni ya chini ya ardhi huko Brooklyn, mjini New York Jumanne asubuhi.

Naibu Kamishna wa Kwanza wa Idara ya Zimamoto ya New York Laura Kavanagh alisema watano kati yao wako katika hali mbaya.

Polisi imesema muda mfupi kabla ya saa 2:24 asubuhi kwa saa za New York, treni ilipokuwa ikiingia kwenye Kituo cha 36th Street katika eneo la Sunset Park, mwanamume mmoja aliyevalia kizibao cha ujenzi na barakoa ya kuzuia gesi aliwafyatulia risasi watu wengi kwenye treni na jukwaa la karibu.

Kamishna wa Polisi wa Jiji la New York Keechnat Sewell alisema kwa sasa hakuna vifaa vya vilipuzi vinavyopatikana kwenye treni za chini ya ardhi na tukio hili halichunguzwi kama kitendo cha ugaidi kwa wakati huu, akiongeza kuwa maafisa bado hawajatambua nia ya shambulizi hilo.