Watu 9 wafariki katika tukio la mkanyagano wa mkesha wa mwaka mpya nchini Uganda
2023-01-02 08:36:26| cri

Polisi nchini Uganda wamesema, watu tisa wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tukio la mkanyagano lililotokea kwenye jumba la maduka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala, kwenye mkesha wa mwaka mpya.

Polisi pia wamesema, baadhi ya waliofariki ni vijana walioshiriki katika onyesho la muziki usiku huo. Tukio hilo lilitokea usiku wa manane wakati waandaji wa sherehe kuwahimiza washiriki kwenda nje kutazama onyesho la fataki.