Msomi wa Afrika aeleza matumaini mazuri kwa uchumi na maboresho ya sera ya China kuhusu COVID-19
2023-01-02 08:50:01| CRI

Msomi wa Uhusiano wa Kimataifa kutoka nchini Kenya Cavince Adhere amesema, uchumi wa China umedhihirisha unyumbufu na uvumbuzi, huku akielezea matumaini mazuri kwa uchumi wa nchi hiyo kwa mwaka huu baada ya China kufanya maboresho ya sera zake kuhusu janga la COVID-19.

Akizungumza na Shirika la Habari la China Xinhua hivi karibuni, msomi huyo amesema kuna ishara zote kuwa uchumi wa China utaendelea kukua katika mwaka huu.

Amesema Mkutano wa Kazi za Uchumi uliomalizika hivi karibuni nchini China umesisitiza nafasi ya matumizi katika maendeleo ya uchumi na nafasi ya uvumbuzi katika mageuzi ya kiuchumi.

Ameongeza kuwa Afrika ina matarajio mazuri ya mwaka mwingine wa uhusiano wa karibu wa kiuchumi na China, nchi ambayo imekuwa mwenzi mkubwa wa biashara kwa bara hilo tangu mwaka 2009.