Kiongozi wa Sudan athibitisha kujiondoa kwa jeshi katika mchakato wa kisiasa
2023-01-02 08:40:48| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amesisitiza dhamira ya jeshi la nchi hiyo ya kujiondoa katika mchakato wa kisiasa nchini humo.

Al-Burhan amesema hayo katika hotuba aliyoitoa katika maadhimisho ya miaka 67 ya Uhuru wa Sudan.

Amesisitiza dhamira ya jeshi la nchi hiyo kujitoa kabisa katika mchakato wa kisiasa, na dhamira ya ulinzi wa kipindi cha mpito ili kukabiliana na majaribio ya mapinduzi na mahitaji ya kipindi cha mpito.

Pia ameeleza matumaini yake kuwa serikali ya mpito itaundwa ili kutafuta ufumbuzi wa dharura wa matatizo ya kiuchumi, ujenzi wa amani, kutimiza usalama na utulivu, na kufanya maandalizi kwa ajili ya uchaguzi.