Sudan Kusini yaeleza matumaini kuhusu uondoaji wa vikwazo vya UM dhidi yake
2023-01-02 08:36:17| cri


 

Sudan Kusini hivi karibuni ilieleza matumaini yake kuwa, Umoja wa Mataifa utaondoa marufuku ya silaha na vikwazo dhidi ya nchi hiyo na baadhi ya maofisa wa serikali yake.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini Deng Dau Deng amesema, serikali inafanya jitihada ili kufikia vigezo vitano vya kuondoa vikwazo, marufuku ya silaha na vikwazo dhidi ya watu binafsi.

Vilevile ameutaka Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kimataifa kuunga mkono uondoaji wa vikwazo na marufuku ya silaha dhidi ya nchi hiyo.