Katibu mkuu wa UM asikitishwa na mlipuko mbaya wa gesi nchini Afrika Kusini
2023-01-03 08:23:44| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezwa kusikitishwa kwake na vifo vya raia vilivyotokana na mlipuko wa tanki la gesi katika mji wa Boksburg, jimbo la Gauteng, nchini Afrika Kusini.

Msemaji wa Katibu Mkuu huyo, Stephane Dujarric amesema, Bw. Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu, kwa serikali na watu wa Afrika Kusini, na kuwatakia majeruhi wapone haraka.

Katika mlipuko huo, watu 34, wakiwemo wahudumu 11 wa afya katika hospitali iliyo karibu na eneo la tukio walifariki.