Rais wa China amtumia barua ya pongezi Luiz Inácio Lula da Silva kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Brazil
2023-01-03 08:26:49| CRI

Rais wa China Xi Jinping amemtumia barua ya kumpongeza Luiz Inácio Lula da Silva kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Brazil.

Rais Xi amesema, katika miaka 48 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Brazil, chini ya juhudi za pande zote mbili, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiimarishwa na kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa uhusiano kati ya nchi kubwa zinazoendelea.

Pia amesisitiza kuwa, ataendelea kuhimiza uhusiano wa kiutendaji kati ya pande mbili, kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati katika pande zote hadi kufikia kiwango cha juu zaidi, na kuzinufaisha zaidi nchi hizo mbili na wananchi wao.