Burundi yatangaza mlipuko wa kipindupindu
2023-01-03 08:25:48| CRI

Waziri wa Afya ya Umma na Udhibiti wa UKIMWI nchini Burundi, Sylvie Nzeyimana jumapili jioni ametangaza mlipuko wa kipindupindu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura.

Katika taarifa yake, Waziri Nzeyimana amesema, kesi tisa zinazoshukiwa kuwa na ugonjwa huo zilitambuliwa Desemba 30, 2022 katika eneo la kaskazini mwa mji wa Bujumbura, hususan katika kata za Bukirasazi na Kinama, na siku mbili baadaye, kesi mbili ziliripotiwa katibu na eneo la Mutakura.

Mlipuko wa kipindupindu umetokea baada ya mvua kubwa kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bujumbura kuanzia Desemba 26 hadi 31, 2022, na kusababisha vyoo vingi kujaa maji.

Wizara ya Afya ya Burundi pia imepiga marufuku uuzaji wa chakula kilichopikwa na bidhaa za chakula katika mitaa ya mji wa Bujumbura kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo.