Wanajeshi wa Israel waua wapalestina wawili katika ukingo wa magharibi wa Mto Jordan
2023-01-03 08:12:59| cri

Wizara ya Afya ya Palestina jana ilitoa taarifa kuwa, wanajeshi wa Israel wamewaua raia wawili wa Palestina na kujeruhi wengine watatu katika mji wa Jenin.

Mashuhuda wa tukio hilo wameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwamba, wanajeshi hao waliingia katika kijiji kimoja magharibi mwa Jenin na kulipua nyumba mbili na kupambana na wapalestina wanaoishi katika eneo hilo.