Rais wa Malawi kutangaza baraza dogo la mawaziri
2023-01-03 08:24:41| CRI

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesema anatrajia kutangaza baraza dogo la mawaziri hivi karibuni, linalolenga kutumia vizuri rasilimali zilizoko ndani ya nchi.

Rais Chakwera amesema hayo katika ujumbe wake wa Mwaka Mpya uliotangazwa kwenye vituo vya televisheni nchini humo jumapili jioni, na kuongeza kuwa uundaji wa baraza lake jipya la mawaziri uko katika hatua za mwisho, na ofisi yake itatoa tangazo baadaye mwezi huu.

Amesema Wamalawi watarajie baraza dogo la mawaziri linalolenga kuboresha huduma zinazotolewa kwa jamii, kasi kubwa katika miradi ya kijamii ambayo ujenzi wake unaendelea, na kufungua sekta nyingine za kiuchumi nchini humo zenye fursa nyingi za kiuchumi kwa ajili ya ukuaji jumuishi na ustawi wa pamoja, hususan katika sekta za kilimo, utalii na madini.