Rais wa Msumbiji aahidi kulinda amani na usalama wa kimataifa
2023-01-04 08:29:34| CRI

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ameahidi kulinda amani na usalama wa kimataifa wakati nchi hiyo ikianza kipindi cha miaka miwili kama nchi asiye mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wa Facebook, rais Nyusi amerejea tena mwongozo wa nchi hiyo unaolenga kulinda na kudumisha matakwa ya Msumbiji, Afrika, nchi zinazoendelea na dunia kwa ujumla ili kuboresha ustawi na maendeleo endelevu ya binadamu wote.

Amesema tukio hilo halijawahi kutokea katika historia ya Msumbiji, na ni ushahidi wa imani na hadhi ya Msumbiji kati ya nchi nyingine duniani.

Msumbiji ilichaguliwa kuwa nchi mjumbe asiye wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2023 na 2024 katika kikao kilichofanyika mwezi Juni mwaka jana.