Nchi nyingi zalaani waziri wa usalama wa Israel kuingia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa
2023-01-04 08:30:15| cri

Waziri mpya wa usalama wa Israeli, Bw. Itama Ben-Gevir jana aliingia kwenye viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa katika Mji Mkongwe wa Jerusalem, kitendo kilicholaaniwa vikali na Palestina na nchi nyingine. .

Katika taarifa yake, Bw. Ben-Gevier amesema kabla ya kuingia kwenye eneo hilo, alifanya tathmini kwa kushirikiana na polisi wa Israeli na mashirika ya usalama wa kitaifa na kupata idhini. Pia alisisitiza kuwa serikali mpya ya Israel haitakubali tishio kutoka kundi la Hamas.

Habari zinasema, Bw. Ben Gevir alikaa kwenye eneo la nje la Msikiti wa Al-Aqsa kwa takriban dakika 15, lakini hakuingia ndani ya Msikiti huo.