Idadi ya vifo katika gereza nchini Mexico yafikia 17
2023-01-04 08:27:45| CRI

Idadi ya vifo kutokana na shambulizi lililotokea ndani ya gereza moja lililoko mjini Ciudad Juarez, mkoa wa Chihuahua kaskazini mwa Mexico imeongezeka na kufikia 17, wakiwemo walinzi 10 wa gereza hilo.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini humo imesema katika taarifa yake kuwa, jumla ya wafungwa 27 wametoroka wakati wa tukio hilo, na watu wengine 13 wamejeruhiwa, wakiwemo wafungwa 10 na maofisa watatu.

Waziri wa Ulinzi wa Mexico Luis Cresencio Sandoval amesema, msako katika gereza hilo uligundua vyumba 10 vya anasa ndani ya gereza, silaha, dawa za kulevya na zaidi ya dola za kimarekani 87,000 zilizowekwa katika kabati la kuhifadhi fedha.

Pia Waziri huyo amesema, watu walioshambulia gereza hilo ni wafuasi wa kundi la kihalifu la Los Mexicles, na miongoni mwa wafungwa waliotoroka ni kiongozi wa kundi hilo Ernesto Alfredo Pinon.