China kuboresha zaidi hatua za kukinga na kudhibiti COVID-19 ili kuhakikisha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa
2023-01-04 08:32:04| cri


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema, China itaendelea kuboresha hatua za kukinga na kudhibiti janga la COVID-19 kwa mujibu wa hali ya janga hilo, kuweka masharti mazuri zaidi kwa mawasiliano ya watu wa ndani na nje ya nchi, na kuhakikisha ushirikiano na mawasiliano ya kimataifa.

Vilevile amesema China na Shirika la Afya Duniani (WHO) zilifanya mkutano kwa njia ya video, ambapo pande hizo mbili zilibadilishana maoni kuhusu hali ya janga, matibabu, na chanjo, na kukubaliana kuendelea na mawasiliano ya ufundi, na kusaidia kukomesha janga hilo mapema.