Msomi wa Kenya asema marekebisho ya China kuhusu sera ya kuzuia janga la COVID-19 yatanufaisha uchumi wa dunia
2023-01-04 08:33:00| CRI

Msomi wa masuala ya mambo ya kimataifa wa Kenya Cavince Adhere amesema, marekebisho yaliyofanywa na China hivi karibuni China kuhusu sera ya kuzuia na kudhibiti COVID-19 yamefanyika kwa wakati mwafaka.

Amesema hatua hiyo imeonesha kuwa kinga na udhibiti wa janga hilo nchini China umeingia katika kipindi kipya, hali itakayonufaisha uchumi wa dunia, na kuongeza kuwa, anaamini kuwa marekebisho ya sera hizo yataleta matokeo chanya kwa maendeleo ya utalii nchini China na sehemu nyingine duniani.

Amesema kutokana na utekelezaji wa sera mpya, sekta ya utalii ya Kenya ina matumani makubwa ya kuvutia tena idadi kubwa ya watalii kutoka China.

Aidha, Cavince amesema nchi zote zinatakiwa kushirikiana kuhimiza ufufukaji wa uchumi duniani, na kukaribisha mustakabali mzuri.