Watu 28 wauawa nchini Burkina Faso
2023-01-04 08:31:39| CRI

Watu 28 wameuawa mkoani Kossi, kaskazini mwa Burkina Faso katika usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi.

Msemaji wa serikali ya nchi hiyo Jean-Emmanuel Ouedraogo amesema, tukio hilo lilitokea katika mji mkuu wa Kossi, Nouna, na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kugundua mazingira ya mauaji hayo na kuwatambua wahusika.

Amesema tukio hilo limetokea wakati Burkina Faso ikifanya jitihada za kuwakusanya watu ili kuchukua hatua za pamoja katika kupambana na ugaidi.