Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ateua kamanda mpya wa kikosi cha kulinda amani nchini DR Congo
2023-01-05 08:20:53| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amemteua Luteni Jenerali Otávio Rodrigues De Miranda Filho wa Brazil kuwa kamanda mpya wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO).

Miranda Filho anachukua nafasi ya Luteni Jenerali Marcos de Sá Affonso da Costa wa Brazil, ambaye atakamilisha majukumu yake Februari 28.