Umoja wa Mataifa watoa dola za kimarekani milioni 7 kusaidia watu 423,000 nchini Mali
2023-01-05 08:21:11| cri


 

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric jana amesema, Mfuko wa Kukabiliana na Dharura wa Umoja wa Mataifa utatoa dola za kimarekani milioni 7 kwa watu wanaokabiliwa na ukosefu wa usalama nchini Mali.

Msemaji huyo amesema, mahitaji ya kibinadamu nchini Mali ni makubwa, kwani nchi hiyo inakabiliwa na mgogoro wa pande nyingi. Ameongeza kuwa, katika mwaka huu, dola za kimarekani milioni 868 zinahitajika kusaidia watu milioni 6.2 nchini Mali.