Nchi za magharibi zakosolewa kwa kushambulia mwongozo wa China wa kudhibiti Covid 19
2023-01-06 09:37:21| cri
Msomi anayefuatilia maswala ya China na Afrika Dkt. Cliff Mboya anasema China ina haki ya kufuata mwongozo wautakao katika kupambana na virusi vya COVID-19.
Mboya ameiambia Radio China Kimataifa kwamba awali nchi za magharibi zilikuwa zinakosoa juhudi za China za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona bila kuwa na ufahamu kuwa kila nchi inaweka sera kulingana na hali yake halisi.
Anaongeza kuwa China imeonyesha kuwa inaujali ulimwengu na ndio maana imekuwa ikizisaidia nchi za Afrika ili kwa pamoja kutokomeza virusi vya Corona. Kauli hii inakuja siku moja tu baada ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin kukosoa vyombo vya habari vya magharibi kwa kuchafua rekebisho la sera ya China ya kudhibiti na kukinga janga la COVID-19.

Bw. Wang amesema, tangu mlipuko wa janga hilo utokee miaka mitatu iliyopita, serikali ya China siku zote inashikilia kuweka kipaumbele wananchi na maisha yao.