Rais wa Afrika Kusini aahidi kutatua changamoto za nishati, kupambana na uhalifu na ufisadi
2023-01-09 08:51:30| CRI

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameahidi kutatua changamoto za nishati na kuimarisha juhudi za kupambana na uhalifu na ufisadi.

Rais Ramaphosa ambaye pia ni kiongozi wa Chama tawala cha ANC, ametoa kauli hiyo alipohutubia maadhimisho ya 111 ya Chama hicho kwenye uwanja wa michezo wa Dr. Petrus Molemela huko Mangaung, mkoani Free State.

Rais Ramaphosa amesema serikali inapaswa kutoa kipaumbele katika kuwekeza zaidi kwenye miundombinu kuliko matumizi mengine, pamoja na kuendeleza mageuzi ya kimfumo ya sekta za mtandao, ikiwemo umeme, mawasiliano ya simu, maji, reli, usafiri wa ndege na miundombinu ya barabara.