Mfumo wa bima wa China kuhusisha dawa zaidi za kupambana na COVID-19
2023-01-09 08:20:11| CRI

Idara ya usalama wa afya ya taifa ya China (NHSA) imesema majadiliano kuhusu dawa zinazoweza kuhusishwa kwenye mfumo wa taifa wa bima ya matibabu yamekamilika, na dawa mbili za kupambana na COVID-19 zimeongezwa.

Kwenye majadiliano ya muda wa siku nne, dawa za aina Paxlovid ya kampuni ya Pfizer, dawa ya Azvudine na dawa moja ya mitishamba zilijadiliwa, na hatimaye dawa ya Azvudine na dawa ya mitishamba ziliidhinishwa kuwekwa kwenye orodha. Hadi sasa kuna dawa zaidi ya 600 kwenye mfumo huo.

Wakati huo huo kituo cha kupambana na maradhi cha China (China CDC) kimesema virusi vya Omicron aina ya XBB, kwa sasa haviwezi kusababisha wimbi kubwa la maambukizi nchini China. Hata hivyo mfumo wa kufuatilia aina hiyo ya virusi umeimarishwa.