Rais wa Brazil alaani uvamizi wa wafuasi wa Bolsonaro dhidi ya vyombo vya mamlaka ya nchi
2023-01-09 09:13:27| CRI

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil amelaani uvamizi wa wafuasi wa rais wa zamani Jair Bolsonaro uliofanywa jana kwenye bunge, ikulu na Mahakama kuu, na kusema wafuasi hao wataadhibiwa kisheria.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti kuwa vikosi vya usalama vya Brazil vimedhibiti tena jengo la bunge la taifa kutoka kwa waandamanaji hao, wakati operesheni bado zinaendelea katika makao makuu ya Mahakama kuu na ofisi za Ikulu.