UNICEF yasafirisha tani 30 za vifaa tiba kwenda nchini Somalia
2023-01-10 09:15:10| CRI

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema limesafirisha takriban tani 30 za dawa na vifaa tiba ili kusaidia huduma za afya za kuokoa maisha katika maeneo yaliyoathirika zaidi nchini Somalia.

Mwakilishi wa shirika hilo nchini Somalia Bibi Wafaa Saeed Abdelatef amesema watoto na wanawake wanachukua zaidi ya asilimia 80 ya watu waliopoteza makazi yao nchini Somalia, watoto ni miongoni mwa walioathirika zaidi, huku milioni 5.1 wakihitaji msaada wa kibinadamu. Pia amesema changamoto hizi zinaambatana na milipuko ya magonjwa ya kipindupindu na surua, ambayo imefanya hali izidi kuwa mbaya.