China yatoa mwito wa utekelezaji kamili wa azimio kuhusu utoaji msaada wa kuvuka mpaka kwenda Syria
2023-01-10 08:39:24| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun, ametoa mwito wa kufanywa juhudi za kuhakikisha utekelezaji kamili na wenye ufanisi wa azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu utoaji msaada wa kuvuka mpaka nchini Syria.

Balozo Zhang amesema China inatumai kuwa Baraza la Usalama na Mashirika husika ya Umoja wa Mataifa yatatumia fursa ya uzoefu na upungufu uliopo kwenye utekelezaji wa azimio namba 2642 katika muda wa miezi sita iliyopita, ili kuhakikisha utekelezaji kamili na wenye ufanisi wa azimio namba 2672 na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuendelea kuboresha hali ya kibinadamu kwa wasyria wote.

Balozi Zhang pia amesisitiza kuwa ukamilifu wa ardhi ya Syria na umiliki wake vinatakiwa kuheshimiwa.