Reli ya Ethiopia Djibouti yaingiza dola za kimarekani milioni 47.4 katika miezi minne iliyopita
2023-01-10 08:40:04| CRI

Ofisa mkuu mtendaji wa Shirika la Reli ya Ethiopia-Djibouti (EDR) Bw. Abdi Zenebe, amesema shirika hilo limepata takriban dola za kimarekani milioni 47.4 katika kipindi cha miezi mitano iliyopita.

Bw. Zenebe amesema reli hiyo yenye urefu wa kilometa 752.7 iliweza kusafirisha tani laki 5 za mizigo na kufanikiwa kuingiza kiasi hicho cha fedha, ambacho ni ongezeko la Birr Milioni 600 za Ethiopia ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka EDR utendaji wa reli hiyo katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, umechangia ongezeko la usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi kwa asilimia 11.2 na uagizaji kwa asilimia 15. Bidhaa zilizosafirishwa zaidi nje ni pamoja na mbolea, mafuta ya kula, ngano na magari.