Waziri wa mambo ya nje wa China afanya ziara barani Afrika
2023-01-10 16:59:31| CRI


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin ametangaza kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang atafanya ziara nchini Ethiopia, Gabon, Angola, Benin, Misri, na makao makuu ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kiarabu.

Amesema ziara hiyo inayoanza tarehe 9 hadi 16 mwezi huu, inalenga kukuza zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Afrika katika pande zote, na kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Huu pia ni mwaka wa 33 mfululizo kwa waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara yake ya kwanza ya mwaka mpya barani Afrika.